Deuteronomy 24:1-4

Sheria Kuhusu Ndoa Na Talaka

1 aIkiwa mtu atamwoa mke na akamchukia kwa sababu ya kukosa adabu, naye akamwandikia hati ya talaka, akampa na kumfukuza kutoka nyumbani kwake, 2ikiwa baada ya kuondoka nyumbani kwake atakuwa mke wa mtu mwingine, 3ikiwa mume wake wa pili atachukizwa naye akamwandikia hati ya talaka, akampa na kumfukuza kutoka nyumbani kwake, au kama akifa, 4 bbasi yule mume wake wa kwanza, ambaye alimpa talaka, haruhusiwi kumwoa tena baada ya mwanamke huyo kuwa najisi. Hayo yatakuwa machukizo machoni pa Bwana. Usilete dhambi juu ya nchi ambayo Bwana Mwenyezi Mungu wako anakupa kama urithi.

Copyright information for SwhKC